Loading...

Injili ya Kidigitali
Kwa Kizazi cha Sasa

Tunaandaa mifumo ya kidigitali kwa ajili ya Injili — kutoka kuhubiri Kanisani hadi Biblia Ai, Mifumo ya kisasa ya kidijitali na msaada wa kuhubiri kwa ufanisi mtandaoni bure. Karibu uchangie sadaka yako kueneza Neno mtandaoni, kufundisha wanafunzi wa Kristo, na kusaidia makanisa yenye njaa ya kiroho kukua kiteknolojia.

Digital Gospel Illustration - Kanisa Network

Hatutengenezi tovuti za bure pekee, bali tunajenga madhabahu za kidigitali kwa ajili ya makanisa.

Kanisa Network ni harakati ya kidigitali inayoleta Injili mahali ambapo vijana na familia nyingi za sasa wanaishi: WhatsApp, TikTok, Simu, AI, na mitandao yote ya kijamii.

KanisaGPT

Tunasaidia makanisa kufundisha Biblia kupitia KanisaGPT - mfumo wa akili bandia unaojibu maswali ya kiroho na kusaidia ufahamu wa Biblia. (Tupo kwenye mchakato wa kuukamilisha)

Mtaa Messenger

Tunapeleka maombi, SMS, na mafundisho kwa maelfu kupitia Mtaa Messenger - mfumo wa ujumbe wa moja kwa moja wenye kufuatilia ukuaji wa waumini kiroho.

Ufundishaji kwa mtandao

Tunawasaidia wachungaji kufikia kizazi kilichopotea kupitia njia ya mtandao bure, bila gharama kubwa za teknolojia wanaweza kufikisha ujumbe wao kwa mataifa.

Sadaka Yako Inawezesha Nini?

Kila shilingi unayotoa inasaidia kueneza Injili kwa njia mpya za kidigitali.

TZS 30,000

Kurasa (Landing page) kwa huduma moja pia upatikanaji katika ramani za Google

TZS 75,000

SMS 300+ kwa huduma kufikia watu katika eneo lake na kufuatilia ukuaji wa kiroho

TZS 100,000

Vifaa na mafunzo ya huduma moja kuhusu uinjilisti wa mtandaoni

TZS 250,000+

Kukuza na kukamilisha KanisaGPT; kufundisha Biblia na kujibu maswali ya kiroho

"Toa kwa hiari, jenga kwa upendo, eneza kwa Neno."

Changia Sadaka Sasa

Ushuhuda wa Mavuno

Makanisa na wachungaji wamebadilika kupitia mfumo wetu wa kidigitali.

"Nilifikiria Injili mtandaoni ni kwa makanisa makubwa, hadi tulipopata msaada kutoka Kanisa Network. Sasa tunaweza kufikia vijana wetu kila wiki kupitia Mtaa Messenger."

D

Pastor D.

Arusha

"KanisaGPT imebadilisha kabisa namna tunavyofundisha Biblia. Vijana wanauliza maswali wakati wowote na kupata majibu mara moja. Mavuno ya kiroho yameongezeka sana."

E

Mama Esther

Dodoma

"Kwa msaada wa Kanisa Network, tumeongeza idadi ya vijana wanafunzi kutoka 15 hadi zaidi ya 100 kwa miezi michache tu. Teknolojia imetusaidia kufikia wale ambao hawakuwa na uwezo wa kuja kanisani."

J

Pastor John

Mwanza

"Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi..." — Mathayo 28:19

"Na watawezaje kusikia pasipo mhubiri? ... Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari njema." — Warumi 10:14-15

Tamko la Harakati:

"Hatujengi tovuti — tunachochea uvuvio wa kidigitali. Hatugojei umati uje kanisani — tunapeleka Injili kwao, popote walipo."